19 Machi 2011 - 20:30

Abna inatuhabarisha kuwa:Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa: Jamhuri ya kiislamu ya Iran imefanikiwa kupata teknolojia ya kisasa ya nishati ya nyuklia kutokana na Uimara na misimamo yake.

Rais Ahmadinejad amesisitiza kwamba, hatua ya serikali na wananchi wa Iran ya kusimama madhubuti dhidi ya vitisho na mashinikizo ya Wamagharibi ndio sababu kuu ya maendeleo ya taifa hili. Rais Ahmadinejad amesisitiza kwamba, Iran na wananchi wake wapoimara na kwamba, vitisho au vikwazo abadani haviwezi kulikwamisha taifa hili kufikia malengo yake. Rais Ahmadinejad ametaka kuzidishwe juhudi za kila hali hasa za viongozi wa nchi kwa ajili ya kupeleka gurudumu la Jamhuri ya kiislamu kwenye kilele cha elimu,nguvu na maendeleo.